Suzan Harvey
aka Goldie
Ni taarifa ambayo kila aliekua karibu na Goldie kwenye page zake za
facebook na twitter inakua ngumu kuamini, taarifa rasmi zimeripoti kwamba
Goldie ambae ni mwakilishi wa Nigeria kwenye BBA 2012 AMEFARIKI muda mfupi tu
baada ya kuwasili Lagos Nigeria akitokea Marekani ambapo bado chanzo cha kifo
chake hakijajulikana.
Mmoja wa wasaidizi wake amethibitisha kifo cha Goldie kupitia page ya
twitter ya Goldi kwa kusema ni kweli msanii huyo amefariki dunia usiku wa
february 14 2013 muda mfupi tu baada ya kuwasili Lagos Nigeria.
Taarifa nyingine nilizozipata kutoka kwa mtu wake wa karibu wanaeshirikiana
kimuziki zimeeleza kwamba mpenzi wake Goldie ambae ni Msanii wa Kenya CMB
Prezzo ametua Nigeria usiku huu muda mfupi uliopita kwa ajili ya kuendeleza
mipango aliyokua nayo na Goldie ikiwemo kutengeneza show ya TV.
Prezzo alitakiwa kushiriki katika TV show ambayo yeye na Goldie wangekua
moja ya wahusika wakuu ambapo mpango ulikua baada ya mwezi mmoja Goldie na Prezzo
wangekuja Tanzania, Uganda na Kenya kwa ajili ya kujitangaza na kuipromote
single mpya ya Goldie ya ‘Skibobo’ aliyofanya na AY...

No comments:
Post a Comment