...
Hayo yamesemwa na kaimu mganga mkuu wa serikali Dr.Donan Mmbando wakati wa uzinduzi wa huduma ya teknolojia ya simu kwa ajili ya kupata huduma za afya hasa kwa wajawazito.
Teknolojia hiyo, itamuwezesha mama mjamzito kupewa taarifa za uzazi kupitia simu ya mkononi kwa kuuliza au kujieleza na kupewa majibu yatakayomuwezesha kutafuta kituo cha afya kwa ajili ya kupata matibabu zaidi.
Akiongea katika hafla hiyo Dr.Mmbando amsema kuwa huduma hiyo itasaidia watanzania walio wengi lakini pia kurudisha wafanyakazi wa kuhudumia jamii kwa wingi zaidi na kuondokana na vifo vya mama na mtoto.
Naye mratibu wa program hiyo ambayo tayari imefika nchi za Rwanda na Uganda Glady Someren amesema kuwa kwa kiasi kikubwa wamefanikiwa kuwafikia wananchi waliowengi kutokana na watumiaji wa simu za mkononi kutumika na watu wengi
Hata hivyo serikali imeongeza bajeti ya afya kutoka shilingi billion 271 mwaka 2005 na kufikia shilingi Trillion 1.5 kwa mwaka huu kwa lengo la kuwapatia wananchii huduma za afya katika umbali usiozidi kilomita tano kwa kila wilaya.
No comments:
Post a Comment