Ng'ombe wa
kienyeji ndiyo wanaofugwa kwa wingi Tanzania bara na Visiwani ikiwa ni asilimia
96.2 bara na asilimia 95.2 visiwani.
Ng'ombe wa nyama na maziwa walioboreshwa ni
asilimia (0.9 na 2.9) kwa bara na asilimia (0.7 na 4.1) kwa visiwani. Idadi ya
ng'ombe Tanzania bara na visiwani inaonekana kupongezeka ukilinganisha na ya
sensa ya mwaka 2002/2003 kwa ng'ombe 4,281,082.
Takwimu hizi zinaonyesha kuwa
mkoa wa Shinyanga ndio unaofuga ng'ombe wengi zaidi ikifuatiwa na Tabora. Mikoa
mingine inayofuga ng'ombe wengi kuanzia milioni moja hadi mbili ni Mwanza, Arusha, Mara, Manyara,
Singida and Dodoma.

No comments:
Post a Comment